Thursday, 17 November 2011

WALAHI MUUNGANO ZENJI-BARA NJIA PANDA

Hayawi hayawi ........!

Eti tunasherehekea miaka 50 ya Tanzania! Tanzania ama Tanganyika? CCM inaficha ukweli ili kuzuia harakati za Bara kudai Tanganyika na wana Zanzibar kudai serikali huru!

Unajua Bara watu wengi haswa waliopo vijijini, awajui demockrasia ni nini, na serikali ya CCM inachukulia upenyo huo kuwafumba watu macho na kuwalaghahi kwamba vyama vya upinzani ni chanzo cha vurugu. Ndio maana wabunge wa CCM hawataki maswada wa Katiba uitishwe upya sababu maswala ya muungano yataibuka.

Kwa upande wa Visiwani, mambo ni tofauti yahee! Wajua kwamba vuguvugu za vyama vingi zilianza huko zamani kutokana na wengi kuupinga muungano unaoitwa Tanzania! Kipindi kile wanaharakati wa Zanzibar walitaka kuwa na serikali yao, lakini mfumo ulikuwa tofauti, hivyo wengi walikimbia nchi. Lakini sasa mfumo wa vyama vingi vya siasa umerudi na wao wamepata nafasi ya kurudi nyumbani.

Lakini swala alijaishia hapo! Ni kwamba huko Visiwani vuguvugu la wanaharakati ni kutakala Zanzibar kupewa uhuru kamili kwa madai kwamba muungano huu wa Tanzania si halali. Kuna ukweli ndani ya madai hayo kwani hata upande wa Bara wanaharakati wanataka muungano upitiwe ikiwa ni kurudishwa kwa nchi ya Tanganyika.

Ukweli ni kwamba muungano wa Tanzania una kasoro nyingi, ikiwemo la kutoweka kwa nchi ya Tanganyika yenye serikali yake! Mungano lazima uafikiwe na wengi na nchi usika ziwe na maamuzi yake kwa faida ya pande zote.

Zanzibar kuna kundi linaendeleza harakati za kutaka muungano ufutwe na kudai serikali huru ya Zanzibar, linaitwa Zarfa (Rights of Freedom and Autonomy) wanatarajia kuandamana kesho tarehe 18 November 2011 saa nane mchana, madhumuni ni kudai uhuru wa nchi ya Zanzibar kutoka kwa mkoloni (Tanganyika), kibali kinasubiriwa ili kufanyika maandamano hayo ( http://www.facebook.com/pages/Say-NO-to-the-Tanzania-Union/199890523384975 )

Sasa ni mwendo mdundo, Tanganyika lazima irudi kwenye ramani na Zanzibar iwe nchi huru. Bungeni wapinzani wanalia na Katiba na Zanzibar mambo yameiva.




No comments:

Post a Comment