Tuesday, 29 November 2011

TANZANIA ISIWEKE REHANI ARDHI KWENYE EAC

Ni vizuri serikali ya Tanzania kuhakikisha ardhi yetu aichukuliwi na mabepari wa nje ya umoja wa EAC.

Samweli Sita amegoma kutia saini mkataba wa EAC (Umoja wa nchi za Afrika Mashariki) unaohusu sera ya ardhi ,ulinzi na mambo ya nje. Na Naibu Waziri wa EAC wa Tanzania, Lazaro Nyarandu ameonya swala la ardhi alipaswi kuwa swala la muungano wa umoja huo ( http://www.mwananchi.co.tz/habari/49-uchaguzi-mkuu/17953-tanzania-yagoma-kutia-saini-sera-ya-ardhi-eac ).

Nini kingine tunaegemea zaidi ya viongozi wetu kusimama kidedea! Umoja wa EAC una faida na hasara zake. Hivyo serikali inabidi kuwa makini, sababu uenda msukumo wa kufanikisha ushirikiano huu unatoka kwa mataifa ya nje, ambayo yamesha jipenyeza kwenye baadhi ya nchi wanachama wa EAC kinyume na ilivyo Tanzania. Mataifa tajiri (mabepari) yata hakikisha sera zao zinapitishwa ili wafanikiwe kumiliki na kufilisi rasilimali za Tanzania.

Ukoloni umebadili jina siku hizi, nchi masikini zinatawaliwa kwa kupewa misaada yenye masharti, na masharti mengine ni kuhakikisha mataifa hayo tajiri yanajipenyeza sehemu wanazotaka!

Viongozi wetu wanastahili kufanya maamuzi yenye busara bila kukurupuka kwa faida ya taifa zima.

Swali: JK  itakubali kutia saini mkataba huo?

No comments:

Post a Comment