Mpaka tukumbushwe ndio tuwajibike!
Tanzania imekuwa desturi ama ni jambo la kawaida kwa kashfa mbalimbali kupotelea hewani bila ya wananchi kuuliza wala kutaka kujua nini ilikuwa hatima ya watuhumiwa! Labda ni sababu ya ukiritimba ama tabia za woga tulizojengewa kutoka kwenye misingi mibaya ya siasa za woga zisizo na uwazi (transparency).
Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza ilitakiwa kuilipa serikali ya Tanzania fidia ya £30m baada ya uchunguzi nchini Uingereza kubaini makosa ya kutoweka kumbukumbu za mauzo ya rada kwa Tanzania, na fidia bado aijalipwa mpaka sasa.
Kwa upande wa Tanzania kesi hiyo bado inarindima na hatma ya watuhumiwa walio usishwa kwenye manunuzi ya rada kutoka kwa BAE System aijajulikana mpaka sasa, na watuhumiwa bado wanapeta.
Kwahiyo kamati ya bunge la Uingereza iliyohusika na uchunguzi wa kesi hiyo inakumbusha serikali ya Tanzania, kuhakikisha watuhumiwa walioushwa kwenye kashfa hiyo ya manunuzi ya rada kwa upande wa Tanzania wanachukuliwa hatua zinazostahili yaani kufikishwa mbele ya pilato.
-for more twanga hapa- http://www.bbc.co.uk/news/uk-politics-15955824
Ile kamati ya bunge la Tanzania iliyofunga safari kwenda Uingereza kufuatilia malipo imeishia wapi na report yao? Sababu kamati ya bunge kwa upande wa Uingereza wameshangazwa malipo hayo hayajafanyika mpaka sasa! Wenzetu huwa wanakwenda na kumbukumbu na wakianza ni mpaka wapate suluhisho!
No comments:
Post a Comment