Consolidated Holding Corporation (CHC) ilianzishwa tarehe 01 October 1997 baada ya NBC kuvunjwa, baadhi ya shughuli zake ni ubinafsishaji na usimamizi wa mashirika ya umma. Na mwaka 2007 shughuli za Presidential Parastatal Sector Reform Commission (PSRC) ziliamishiwa chini ya CHC.
Muda wa shirika hili umekuwa ukiongezwa na bunge na ulitegemewa kwisha 30 June 2011, lakini waziri wa Fedha Mh Mkulo aliongeza muda hadi December 2011. CHC inaongozwa na Board Of Directors ambao ni Mwenyekiti (Chairman) anayeteuliwa na rais, akisaidiana na Wajumbe (Directors) watano (5) wanaoteuliwa na Waziri wa fedha. Pia Waziri wa Fedha anayo mamlaka kisheria juu ya CHC
CHC imesimamia ubinafsishaji wa mashirika mengi mfano Shirika la Usafiri Dar-es-salaam (UDA) ambapo inasemekana taratibu azikufuatwa ikiwa ni pamoja na uuzaji wa hisa (unalloted shares) za UDA kwa Simons Group Co (ambayo inamilikiwa na Prof Juma Kapuya aliyewahi kuwa waziri), na malipo kutokana na mauzo hayo yalilipwa kwenye account za watu binafsi wakiwemo vigogo wa serikali zilizopita.Hili pamoja na mengi yamehusisha shirika hili kwenye ufisadi.
Shirika la CHC kiutaratibu lipo chini ya Waziri wa Fedha ambayo inaongozwa na Mh Mkullo. Na Mh Zitto ni Waziri kivuli wa Wizara ya Fedha upande wa upinzani, na kiongozi wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC).
Mh Zitto katika vikao vya bunge vilivyopita, alisisitiza muda wa shughuli za CHC uongezwe baada 30 June 2011.
Lakini Waziri wa Fedha Mh Mkullo alimshutumu Mh Zitto kwamba yeye na kamati yake ya POAC wameongwa ndio maana wanangangania muda wa CHC uongezwe! Mh Zitto aliapa mbele ya bunge kwamba atajiuzulu kama uchunguzi utathibitisha yeye na kamati yake wamepokea rushwa. Pia Mh Zitto alimtaka Mh Mkullo kuapa mbele ya bunge kwamba atajiuzulu iwapo uchunguzi utathibitisha Mh. Mkullo kuusika na ufisadi ndani ya CHC,lakini pamoja na Spika Anne Makinda kumtaka kuapa, Mh Mkullo alishindwa kufanya hivo!
Wakati yote hayo yanaendelea uchunguzi dhidi ya CHC ulikuwa unafanywa na CAG kufuatia ombi la board ya CHC na kuchunguza tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mh Zitto na Kamati yake (POAC) na report bado aijakamilika.
Tatizo limezuka mara baada ya Waziri wa Fedha kusitisha muda wa Board ya CHC terehe 10 October 2011, wakati report ya CAG aijatoka. Swala hili litamuweka Mh Mkullo kwenye wakati mgumu kwani yeye anayo mamlaka juu ya CHC na kama inachunguzwa alipaswa kuwa mstari wa mbele kupiga vita ufisadi na kusubiri report ya CAG itoke kujua nani atawajibishwa.
Mh Zitto amepinga hatua ya Mh Mkullo, na amedai kwamba anao ushahidi kuhusu ufisadi unao muhusisha Mh Mkullo. Je ni kweli amehusika na sasa anafanya maamuzi kufukia madhambi yanayo muhusu? Jibu analijua mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) Bw Utouh
JK atatoa uamuzi gani kufuatia hatua ya Mh Mkullo, atasubiri report ya Bw Utouh (CAG) itoke ama atamsimamisha kazi, na kuanza uchunguzi mwingine?
No comments:
Post a Comment