Friday, 2 September 2011

ZAKIA MRISHO AWAKILISHA VYEMA TANZANIA

Mtanzania pekee katika michezo ya  World Athletics Championships 2011 yanayofanyika Daegu nchini Korea, Zakia Mrisho ameiwakilisha vizuri Tanzania baada ya kufanikiwa kuingia final ya mbio za wanawake 5000m. Pamoja na juhudi zote alifanikiwa kumaliza nafasi ya 11 kati ya 18.

Katika mbio hizo za 5000m kwa wanawake, wanariadha wa Kenya wamemaliza nafasi ya kwanza na ya pili, na  Ethiopia nafasi ya tatu.

Tanzania inahitaji kufanya kazi ya ziada kuwa na wawakilishi wengi katika michezo ya kimataifa. Hongera Zakia Mrisho kwa kupeperusha bendera ya taifa.

angalia matokeo hapa (list iliyopo chini)- http://daegu2011.iaaf.org/ResultsByDate.aspx?racedate=09-02-2011/sex=W/discCode=5000/combCode=hash/roundCode=f/results.html#detW_5000_hash_f

No comments:

Post a Comment