Kashfa kuhusu Meremeta ililipoibuliwa na Mh. Kabwe kwenye kikao cha budget cha 2010/11 kilichopita, spika Anne Makinda aliikabidhi kamati ya bunge ya Nishati na Madini kuchunguza tuhuma hizo.
Lakini kama inavodaiwa spika Anne Makinda amehamishia uchunguzi huo kwenye ya bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama inayoongozwa na Edward Lowasa ambaye ni mbunge wa CCM, na aliyewahi kushika nyadhifa serikalini.
Ikumbukwe kwamba tuhuma hizo zinahusisha TPDF iliyoko chini ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi La kujenga Taifa , na sasa Tume ya Bunge ya Ulinzi na Usalama imekabidhiwa kuichunguza kashfa ya TPDF! Hivyo wasiwasi ni kwamba hakuta kuwa na uwazi kiuchunguzi na utoaji wa report .
TPDF iliingia mkataba (wa 50%- 50% ) na Nedco ya Africa Kusini , kuanzisha mradi wa uchimbaji madini. Nedco ikaishauri TPDF kuchukua mkopo wa $10m kutoka Ned- Bank ya Afrika kusini (yenye uhusiano na Nedco). Lakini mradi aukupata faida ndipo serikali ya Tanzania kupitia Bank of Tanzania (BoT) ikachukua jukumu la kulipa ule mkopo wa $10m kwa Ned-Bank ya Afrika ya kusini.
Kutokana na mkataba ulivyo mgao wa faida ama hasara ni 50% kwa TPDF na 50% kwa Nedco! Hivo tatizo ni la kwanza ni kwanini BoT imelipa deni lote badala ya kulipa nusu kama mkataba unavyodai, na pili kiasi halisi kilicholipwa na BoT kilikuwa $132m, hapo utata mwingine ni ziada ya $122m
TPDF imekuwa na miradi mingi, madai ni kwamba kwanini aikaguliwi (be audited), na kwa hili la Meremeta sababu zilizotolewa ni kwamba mradi ulihusisha mambo ya usalama wa taifa. Hata hivo fedha zilizolipwa zimetoka kwenye kodi za wananchi, na wanastahili kupewa jibu kama waheshimiwa wabunge walivodai.
(more upadates to come)
No comments:
Post a Comment