Msemaji mkuu wa ikulu Mr Salva Rweyemamu amekanusha tuhuma za Wikileaks zinazomuhusisha raisi Kikwete, na kudai kwamba tuhuma hizo ni uzushi na wenye nia ya kuchafua jina la raisi.
Mtandao wa Wikileaks ulidai kwamba JK wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika serikali iliyopita, alisafiri kwenda London kufanya shopping na baadhi ya vitu alivyonunua ni nguo za suti (Saville Row suits ), na garama zote zililipwa na mmiliki wa Kilimanjaro-Kempiski Hotel. Pia mtandao huo umedai kwamba mmiliki huyo alitoa USD million 1 kama mchango garama za kampaini ya uraisi 2005 kwa chama tawala (CCM).
Mtandao huo ulichapisha habari za tuhuma hizo weekend, zilizonukuu nyaraka za siri za mwaka 2006 za balozi wa US nchini Tanzania. Nyaraka hizo za siri zilimnukuu Ms.Lisa Pile ambaye ni publicity director wa Kilimanjaro-Kempiski Hotel kuwa alimfahamisha balozi huyo wa US nchini Tanzania kuhusu safari ya JK kwenda London na garama hizo kulipwa na tajiri huyo,na kwamba mmiliki huyo kwa upande mwingine angepata haki ya kujenga hotel kwenye eneo la Ngorongoro, na ndani ya hifadhi ya Serengeti. Hata hivyo Ms.Pile amekanusha habari hizo na kutaka aombwe radhi.
Msemaji wa ikulu amekanusha vikali habari hizo, akisema serikali inalo fungu za mavazi ya raisi na kwamba raisi ausiki na upokeaji fedha za campaign za CCM. Pia amesema JK amepinga ujengaji wa hotel kuzunguka hifadhi ya Ngorongoro kwa sababu ya kulinda mazingira.
for more- http://www.thecitizen.co.tz/news/4-national-news/14454-ikulu-refutes-wikileaks-claims-on-jk
No comments:
Post a Comment