Thursday 10 January 2013

UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME - SABABU ZAKE

Wewe ni mwanaume? Kama ndio je: huwa unaoga kwa kutumia maji moto? Unakulaga chips, sausage,barger, nyama na maziwa kwa wingi na unapakataga laptop yako mapajani?

Wataalamu wanaendelea na utafiti wao na wametoa baadhi vitu vinavyochangia upungufu wa nguvu za kiume.

Sababu ya kudhoofika kwa mbegu zimetajwa kuwa ni kubadilika kwa hali ya maisha na mazingira.

Imeelezwa kwamba wafanyakazi wa mashambani wanaweza kuathirika kutokana na madawa yanayotumika mashambani. Pia uendeshaji wa vyombo vya moto kwa kuvikalia na upakataji wa computer mapajani kwa muda mrefu.

Wanaume wanashauriwa kupunguza uvutaji sigara, unywaji pombe, ulaji wa vyakula vya kukaanga . Chips, barger, sausages, uchangia kuharibika kwa nguvu za kimume kwa asilimia 43. Pia wanashariwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto na kuacha kuvaa nguo za ndani zinazobana ili kuwezesha mwili kupata hewa.

Pia wanaume wanashauriwa na kupunguza ulaji mirungi (aka miraa), nyama na maziwa, na badala yake waongeze ulaji mboga za majani na matunda,

Wanaume wanashauriwa kula maharage ya soya (yanayo ostrogen inayeongeza testosterone inayosaidia kuzalisha mbegu za kiume), tangawizi na matikiti maji.

Kujua zaidi twanga link - http://www.mwananchi.co.tz/habari/-/1597578/1662328/-/item/0/-/h205arz/-/index.html

No comments:

Post a Comment