Saturday 19 May 2012

MWENGE WA OLYIMPIC WAANZA MBIO ZAKE UK

Mbio za mwenge wa Olympic (Olympic tourch) zimeanza rasmi safari ya siku 70 huko Land's End, Cornwall nchini UK.

Mwenge huo wenye matundu 8,000 unatarajiwa kubebwa na jumla ya watu wapatao 8,000, kwa jumla ya umbali wa mile zipatazo 8,000. Wabebaji hao walioteuliwa watakabidhiana mwenge huo kila baada ya umbali wa mita 300.

Mbio hizo zitapita vitongoji mbali mbali na kufika tamati yake tarehe 27 July 2012, kwenye Olympic Stadium eneo la Stratford, mjini London, siku ambayo michezo ya Olympic itaanza rasmi.

Historia ya Mwenge huu ilianza mwaka 1932 mjini Berlin nchini Ujerumani.

Historia ya kuwashwa kwa moto wa Olympic ilianza nchini Greece, kuashiria kuanza kwa mashindano ya Olympic, ambapo moto huo uliwashwa kwa muda wote wa mashindano. Muendelezo wa historia hiyo ulifanyika kwenye michezo ya Olympic ya mwaka 1928, iliyofanyika Amsterdam

Mwenge huu ulikabidhiwa rasmi kwa UK siku ya Alhamisi, 18 May kwenye mji wa Athens, Nchini Greece.

Kwa jumla michezo hii inatarajiwa kuingiza pato kubwa na kuitangaza UK kona zote za dunia.

Tanzania inastahili kujifunza namna ya kuhamasisha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kupitia mbio za Mwenge wa Uhuru na kutoa taarifa za mafanikio kwa uwazi kwa faida ya taifa zima. 

No comments:

Post a Comment