Friday 4 November 2011

USHOGA NA MSIMAMO WA TANZANIA

Serikali ya Tanzania imesema aitapitisha sheria za kutambua mashoga kwa masharti ya kupewa misaada na Serikali ya Uingereza. Tamko limetowa na viongozi wa bara na visiwani.

Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein amesema swala la haki za mashoga alikubaliki katika jamii kwahiyo alina lazima ya kupitishwa kisheria.

Kwa upande wa bara  waziri wa mambo ya nje na mahusiano ya kimataifa Mh.Bernard Membe amesema Tanzania ipo tayari kusitisha uhusiano na serikali ya Uingereza, kama nchi hiyo itaambatanisha haki za mashoga na misaada. Amesisitiza Tanzania ina tamaduni na sheria zake, na sio vyema kwa nchi tajiri kutoa misaada yenye masharti yasiyo na maadili. Amesema kifungu cha 9(1) cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Tanzania inakataza ndoa ya watu wa jinsia moja.


Kauli hizo zinafuatia masharti yaliyotolewa na waziri  mkuu wa Uingereza kwenye mkutano wa Commonwealth uliofanyika kwenye mji wa Perth nchini Australia ( angalia hapo chini- COMMONWEALTH NA UKOLONI MAMBOLEO ) .Nchi nyingi za Afrika azitambui haki za mashoga kisheria sababu ni kinyume na dini ama tamaduni. Hivyo Tanzania imejiweka kwenye mlolongo wa nchi zilizotoa tamko wazi kupinga kauli ya waziri mkuu wa Uingereza. Nchi nyingine ni Kenya, Uganda, Ghana, Zambia etc.

Rais wa Ghana Mr John Atta Mills alipinga vitisho vya waziri huyo kwa kusema Ghana aitalazimishwa kufuata tamaduni za nje na kusisitiza hataanzisha wala kupitisha sheria ya kutambua mashoga ( http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-15558769 ). 

Zambia nayo imesema aitapitisha sheria ya haki za mashoga  kwa nia ya kupata misaada, bali itapitisha sheria zinazokubalika na wananchi na zanazoendana na tamaduni za nchi hiyo ( http://www.nation.co.ke/News/africa/Zambia+wont+enact+pro+gay+laws+to+get+aid+says+official/-/1066/1266322/-/p01jrt/-/index.html )

Serikali hizi zisisahau kuhusu haki za binadamu za Umoja wa Mataifa (UN), kwani kukubaliana nazo  ni vigumu kukwepa kipengele cha haki za ndoa (Right to Marry)!  Hivyo basi kigezo cha kupinga kupitisha sheria ya haki za mashoga iwe ni kutokana na masharti ya  misaada na sio vinginevyo.

Kitendo cha serikali zetu kutoa misimamo yao kwa sasa si sahihi, bali walitakiwa kufanya hivyo ndani ya mkutano huo ili kuonyesha msimamo na uhodari wao mbele ya waziri mkuu wa Uingereza. Huu ni wakati wa kuelimisha jamii na kusikiliza maoni yao.

No comments:

Post a Comment