Wednesday 7 September 2011

LIBYA- GADDAFI BADO ANAPIGA MISELE!

Waasi wa Libya walitoa siku kumi (10) mpaka jumamosi inayokuja kwa wafuasi wa Gaddafi na wakazi wa eneo la Bani Walid analosadikiwa kiongozi huyo na familia yake kujificha, kujisalimisha na kuruhusu waasi kuingia eneo hilo bila umwagaji damu. Ndani ya siku hizo kumi mazungumzo yamekuwa yakifanyika kujaribu kuepusha vita na maafa.

Wakati mazungumzo yanaendelea, ilifahamika kwamba familia ya Gaddafi akiwemo mke na watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike walikimbilia Algeria. Pia Saif Al-Islam na Gaddafi mwenyewe wamekuwa wakitoa vitisho kwamba watapigana mpaka kufa ili kuikomboa Libya. Huku mtoto mwingine wa Gaddafi akifanya mazungumzo na waasi kuhusu kujisalimisha kwake.

Jumapili iliyopita (4th Sept) ilisikika kwamba msafara wa majeshi na wafuasi wa Gaddafi wameonekana wakisafiri kuelekea jangwa la mji wa Agadez nchini Niger toka kusini mwa Libya, viongozi wa Niger walipinga habari hizo, lakini jana (6 Sept) wamekiri kwamba msafara huo umeingia mji mkuu wa Naimey na kudai kwamba Gaddafi hayupo kwenye msafara huo, lakini yupo Mansour Daw ambaye ni mkuu wa ulinzi wa Gaddafi. Msafara huo ulibeba shehena ya dhahabu na fedha zikiwemo Euros na US-dollars.

Misafara ya wafuasi wa Gaddafi inayoingia Niger inasaidiwa na kabila la Tuaregs nchini Niger. Wito umetolewa na US kwa viongozi wa Niger kuwakamata viongozi wa serikali ya Gaddafi walioingia nchini humo.

Miji yenye wafuasi wa Gaddafi ni pamoja na Bani Walid ambao umezungukwa pande zote na majeshi ya waasi isipokuwa upande wa kusini, na mazungumzo ya kujisalimisha na kuruhusu majeshi ya waasi kuingia kwa amani yanaendela, na siku ya mwisho ni Jumamosi wiki hii la sivyo nguvu za kijeshi zitatumika. Miji mingine ni Sabha, Jufra na Sirte alikozaliwa Gaddafi.

Cha kushangaza , inawezekana vipi mkuu wa ulinzi wa Gaddafi kufika Niger bila ya boss wake (Gaddafi) , na kwanini waasi awakulinda sehemu ya kusini ya mji wa Bani Walid ambako msafara huo ulitorokea, ama walitaka iwe sehemu ya Gaddafi kupitia na baadae akamatwe? Pia kwanini Gaddafi ametorosha shehena ya fedha zote hizo na dhahabu ambazo ni mali ya wananchi wa Libya?

Hata hivo majeshi ya NATO yanauwezo wa kuona chochote kinachoendelea ardhini nchini Libya ikiwemo msafarahuo ulivopita na kujua mawasiliano yanayofanywa ardhini kwa njia ya simu nk. hivyo Niger wasidhani mpango huo aukujulikana tangu mwanzo mpaka yanayoendelea sasa.

Gaddafi na watoto wake watakimbia mpaka lini? Je jumamosi ikifika hatua gani kitafuata!

No comments:

Post a Comment