Wednesday 24 August 2011

GADDAFI ASEMA 'USHINDI AMA KIFO'

Gaddafi ametoa ujumbe kwamba atapigana mpaka ushindi upatikane ama kufa.

Makazi ya kiongozi huyo yapo mikononi mwa waasi, na sherehe za ushindi zinaendelea lakini vitisho vya kiongozi huyo vinawapa wananchi wasiwasi kwani wanataka kuona Gaddafi, watoto wake wanakamatwa.

Inaelekea Gaddafi na wafuasi wake wamejificha kwenye mitaro ardhini inayounganisha vitongoji mbalimbali ikiwemo Rixos Hotel (alipojitokeza Saif  Al-Islam na kuhutubia waandishi wa habari ), mji wa Sirte (alikozaliwa Gaddafi), na Mitiga air base (airport inakodhaniwa Gaddafi angetumia ndege kutoroka lakini waasi wanamiliki kwa sasa).

Rixos Hotel imejaa waandishi wa habari wa kigeni,pia yupo congressman wa US Walter Fontroy na Dr KA Paul wa India. Majeshi ya Gaddafi yanawazuia kutoka eneo hilo. Inadhaniwa kwamba mahitaji muhimu kama maji, umeme na vyakula yakipungua itafanya maisha kuwa magumu hotelini hapo
Ujumbe wa waasi (NTC) chini ya mwenyekiti wao Mustafa. A.Jalil unategemea kufanya kikao nchini Qatar kitakacho wakutanisha na ujumbe wa UK, US, France Turkey na UAE kuzungumzia namna ya kuijenga upya Libya.

Gaddafi aliwaita waasi rats (panya) na sasa waasi wamechukua nchi, na yeye amegeuka kuwa panya kwa kujificha chini ya ardhi na kutoa vitisho! Nani panya kati yake na waasi?

Gaddafi ni kiongozi aliyejijengea sifa Afrika na dunia nzima, leo hii badala ya kutumia busara kusikiliza kilio cha wananchi amegeuka kuwa adui wa amani.

Je Gaddafi amegeuka kuwa Osama? Gaddafi amekuwa madarakani 42yr! Je CCM imekuwa madarakani miaka mingapi?

Je who is next in Afrika after Gaddafi kungolewa, iwe chama ama kiongozi?

http://www.bbc.co.uk/news/world-africa-14632674

No comments:

Post a Comment