Tuesday, 23 April 2013

Mh LEMA ASHINDA RUFAA DHIDI YA MAKADA WA CCM

Mahakama ya rufaa Tanzania imetupilia mbali rufani iliyowasilishwa na makada wa CCM dhidi ya Mh Godbless Lema (CHADEMA).

  

Ushindi 22 April 2013......
 

13 February 2013, makada wa CCM ambao ni Mussa Mkanga, Happy Kivuyo na Agnes Mollel waliwasilisha maombi yao kwenye mahakama hiyo kutaka kupitiwa upya uamuzi wa kesi iliyomrejesha Mh Lema kama mbunge wa Arusha Mjini.

21 December 2012, Mahakama hiyo ya Rufaa ilitoa uamuzi ulio mrejesha Mh Lema kama mbunge wa Arusha Mjini baada ya kuvuliwa wadhifa huo na Mahakama kuu ya Arusha.

Ushindi wa 05 April 2012.......

05 April 2012, Mahakama Kuu ya Arusha ilimvua Mh Lema ubunge huo baada ya kupatikana na hatia ikiwemo ya kutumia lugha mbofu mbofu dhidi ya mgombea ubunge wa CCM, Matilda Buriani kwenye campaign za uchaguzi mkuu wa 2010.

Makada hao wametakiwa kilipa gharama zote za kesi.

Kujua zaidi twanga link  http://chademablog.blogspot.co.uk/2013/04/mahakama-yatupilia-mbali-rufaa-dhidi-ya.html

No comments:

Post a Comment