Pichani kushoto ni Mh Godbless Lema, kulia ni mkoko wa Mh Lema ukiburuzwa baada ya kupakiwa isivyo siku ya vurugu chuoni.
Kifo cha mwanafunzi huyo kilitokea usiku wa kuamkia 24 April 2013 baada ya kuchomwa kisu shingoni karibu na eneo la CDA wakati akitoka kwenye kumbi za starehe pamoja na wenzake.
Kufuatia tukio hilo wanafunzi waliamua kuandamana asubuhi ya 24 April 2013 ili kushinikiza uongozi wa chuo kutoa tamko kuhusu matukio ya uhalifu yanayo wakabili wanafunzi wa chuo hicho.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo akiwasili chuoni kuwatuliza wanafunzi
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo alifika chuoni hapo kuwatuliza wanafunzi hao, lakini matokeo yake mkuu huyo wa mkoa aliishia kuzomewa na gari lake kurushiwa mawe, hali iliyo sababisha kutumika kwa mabomu ya machozi.
Ni siku chache zimepita tangu Mh. Lema ashinde rufani yake dhidi ya kesi ya Makada wa CCM walio taka kumng'oa kwenye kiti hicho cha ubunge wa Arusha Mjini.
Pia Mh Lema ni mmoja wa wabunge watano wa CHADEMA waliozuliwa kuudhuria vikao vya bunge kwa muda kama adhabu kwa madai ya kufanya fujo bungeni.
No comments:
Post a Comment