Thursday, 7 March 2013

UCHAGUZI MKUU KENYA - CORD YATADHARISHA UCHAKACHUAJI WA MATOKEO

Wakati matokeo yakiendelea kutolewa, muungano wa CORD (Coalition for Democracy and Reform) uimetaka tume inayosimamia uchaguzi (IECB) kuhakikisha hakuna uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi.
 
Akiongea kwa niaba ya CORD, mgombea mwenza wa Raila Odinga, Kalonzo Musyoka ametaja baadhi ya matatizo kama kuharibika kwa vifaa vya kupigia na kuhesabia kura na upelekaji wa matokeo ya uchaguzi kwa mikono makao makuu kinyime taratibu.
 
Matatizo mengine ni idadi ya kura zilizo hesabiwa vituoni kuzidi idadi ya wapiga kura na kufukuzwa kwa wasimamizi wa CORD kusimamia zoezi la kuhesabu kura makao makuu (Bomas).
 
Pia Bw Kalonzo amedai kushangazwa kwa idadi ya kura zinazo haribika kupungua ghafla baada ya utumaji wa matokeo kwa njia ya mitandao kusitishwa. Maofisa wa vituo kwa sasa wanapeleka ripoti zao kwa mikono makao makuu badala ya njia ya mitandao...........
 

No comments:

Post a Comment