Saturday, 14 July 2012

KATI YA AMIR KHAN NA DANNY GARCIA ZAIDI?

Amir Khan (25) na Danny Garcia (24) wanaingia kwenye ulingo wa Mandalay Bay Convertion Centre, Las Vegas. Ni pambano la uzito wa Light-Welterweight.

Amir anao mkanda wa WBA, naye Danny anashikilia mkanda wa WBC.

Katika pambano la mwisho (Dec 2011) dhidi ya Lamont Peterson, Amir alipoteza mkanda wake WBA.Pamoja na mapungufu yaliyojitokeza kwenye meza ya waamuzi, iligundulika Peterson alitumia madawa ya kuongeza nguvu (steroids) kabla ya pambano, hivyo Amir kurudishiwa mkanda wake wa WBA.

Mshindi wa pambano hili atatoka kifua mbele akiwa na mikanda ya WBA na WBC

Amir analazimika kushinda ili kuthibitisha akupoteza pambano dhidi ya Peterson. Danny anahitaji ushindi ili kumzawadia baba yake anayepiga domo nje ya ulingo kuliko Danny.

Mpambano ni saa 06:00 aka saa 12 asubihi Jumapili saa za Afrika Mashariki


No comments:

Post a Comment