Monday, 11 June 2012

RAFAEL NADAL AMSAMBARATISHA DJOKOVIC

Baada ya mvua kuvuruga mechi ya final siku ya jumapili, Rafael Nadal amemalizia kiporo hicho leo, kwa kumshinda mbabe Novak Djokovic.

Nadal ameibuka na ushindi wa 6-4, 6-3, 2-6, 7-5, na kujikusanyia ushindi huo wa French Open kwa mara ya 7.

Jumapili, Nadal alifanikiwa kupata set mbili za kwanza bila tatizo, lakini hali ilimwendea kombo pale mvua ilivyo kuwa inaongezeka, kwani Djokovic alianza kuonyesha makali yake na kufanikiwa kushinda set ya tatu. Kuona hivyo Nadal akaanza kutoa lawama kwa wasimamizi kwa kutositisha mchezo.

Hata hivyo leo Djokovic akufurukuta, kwani Nadal alichokifanya ni kukamilisha mchezo na kuchukua taji.

No comments:

Post a Comment