Saturday, 9 June 2012

MARIA SHARAPOVA ASHINDA FAINALI ZA FRECH OPEN

Mwanadada wa Russia, Maria Sharapova ameshinda finali za wanawake za mchezo wa tennis, French Open, zilizofanyika nchini Ufaransa.

Maria Sharapova
Sharapova akifurahia kikombe

Sharapova mwenye umri wa miaka 25, bila ya wasiwasi alimsambaratisha mwanadada wa Italy, Sara Errani kwa ushindi wa 6-3, 6-2.

Sharapova sio tu amefanikiwa kupata ushindi wa French Open, bali anashikilia nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake duniani.

Kesho ni siku ya final kwa upande wa wanaume ambapo wababe wawili wanaoshikilia namba 1 na 2 diniani, yaani Novak Djokovic wa Serbia na Rafael Nadal wa Spain watapambana.

No comments:

Post a Comment